Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia swali la wafuasi (muqallidin) wa Ayatullah Makarim Shirazi kuhusu kufika Baytullah al-Haram na safari ya Hijja ndani ya mwaka huu kwa kuzingatia hali zilizopo, mtukufu huyo alieleza hukumu ya Hijja kama ifuatavyo:
1. Wale ambao mwaka huu wamepata uwezo wa kifedha na kimazingira wa kwenda Hijja, lakini kutokana na hali zilizopo wamepatwa na hofu juu ya safari hiyo (kama hofu ya hatari ya maisha, ukosefu mkubwa wa usalama na mfano wake), basi uwezo wao wa kisheria kwa ajili ya kutekeleza Hijja ya wajibu (Hajjat al-Islam) haujapatikana.
2. Wale ambao uwezo wao ulihusiana na miaka iliyopita, ikiwa sasa wana hofu na wasiwasi wa kiakili kuhusu kwenda Hijja, wanaweza kuahirisha safari hiyo hadi mwaka ujao.
Maoni yako